Brazil wakicheza kwao huko Gremio Arena,
Porto Alegre, Usiku huu wameibamiza France Bao 3-0 katika Mechi ya
Kirafiki ikiwa ni matayarisho yao kwa ajili ya ushiriki wao kama Wenyeji
wa Mashindano ya FIFA ya kombe la mabara yatakayoanza Juni 15.
MAKUNDI:
KUNDI A:
-Brazil
-Japan
-Mexico
-Italy
KUNDI B:
-Spain
-Uruguay
-Tahiti
-Nigeria
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.
Kipind cha Pili, Brazil katika Dakika ya
54 kupitia Mchezaji wa Chelsea Oscar na kupiga Bao la pili katika
Dakika ya 84 baada ya kaunta ataki safi ambayo ilimkuta Neymar
aliempoozea Hernanes, alieingzwa Kipindi cha Pili, ambae alimalizia
kifundi.
Bao la 3 la Brazil lilifungwa na Lucas
Moura katika Dakika ya 93 kwa Penati baada ya Marcelo, ambae aling’ara
sana Mechi hii, kuchezewa faulo na Debuchy.
Ushindi huu ni wa kwanza kwa Brazil
kuifunga France katika Miaka 11 na ni kipigo cha tatu mfululizo kwa
France na sasa kinaleta presha kubwa kwa Kocha wa France Didier
Deschamps.
VIKOSI VILIVYOANZA:
BRAZIL: Júlio César, Dani Alves, Marcelo, David Luiz, Thiago Silva, Luiz Gustavo, Oscar, Paulinho, Fred, Hulk, Neymar
FRANCE: H. Lloris, A. Rami, M. Sakho, J. Guilavogui, Matuidi, D. Payet, M. Debuchy, J. Mathieu, Y. Cabaye, Valbuena, K. Benzema
0 comments:
Post a Comment