SPAIN 1 GERMANY 0 & NETHERLANDS 5 RUSSIA 1!!
MARA YA PILI SPAIN USHINDI 1-0 SHUJAA NI ALVARO MORATA!!
MECHI YA KWANZA MORATA APIGA BAO DAK YA 82 NA HII DAK YA 86!
USIKU HUU, kwenye Mashindano ya UEFA kwa
ajili ya Vijana wa chini ya Miaka 21 kuwania Ubingwa wa Ulaya, EURO
U-21, Mabingwa Watetezi Spain na Netherlands wamefanikiwa kutinga Nusu
Fainali kutoka KUNDI B wakiungana na Italy ambao wametoka KUNDI A.
Kwa mara ya pili, Shujaa wa Spain ni
Straika wa Real Madrid ni Alvaro Morata ambae alifunga Bao pekee na la
ushindi kwa Spain dhidi ya Germany katika Dakika ya 86.
Katika Mechi ya kwanza Spain waliifunga Russia Bao 1-0 kwa Bao la Alvaro Morata katika Dakika ya 82.
Nao Netherlands waliisambaratisha Russia
Bao 5-1 na Wafungaji wao walikuwa ni Wijnaldum, De Jong, John, Hoesen
na Fer huku Bao pekee la Russia likifungwa na Cheryshev.
RATIBA/MATOKEO:
(SAA za BONGO)
KUNDI A:
Israel 2 Norway 2 (5 June)
England 0 Italy 1 (5 June)
England 1 Norway 3 (8 June)
Italy 4 Israel (8 June)
Israel v England ( 11 June, Jerusalem, 19:00)
Norway v Italy (11 June, Tel Aviv, 19:00)
KUNDI B:
Spain 1 Russia 0 (6 June)
Netherlands 3 Germany 2 (6 June)
Netherlands 5 Russia 1 (9 June)
Germany 0 Spain 1 (9 June)
Spain v Netherlands (11 June, Petah Tikva, 19:00)
Russia v Germany (11 June, Netanya, 19:00)
NUSU FAINALI:
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A (15 June, Netanya, 18:30)
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B (15 June, Petah Tikva, 21:30)
FAINALI:
18 June, Jerusalem, 19:00
DONDOO MUHIMU:
-Wachezaji wanaoruhuiwa kushiriki Mashindano haya ni wale waliozaliwa Tarehe 1 Januari 1990 au baada ya hapo.
WASHINDI WALIOPITA:
2011: Spain
2009: Germany
2007: Netherlands
2006: Netherlands
2004: Italy
2002: Czech Republic
2000: Italy
1998: Spain
1996: Italy
1994: Italy
1992: Italy
1990: USSR
1988: France
1986: Spain
1984: England
1982: England
1980: USSR
1978: Yugoslavia
WACHEZAJI BORA WA MASHINDANO YALIYOPITA:
2011: Juan Mata (Spain)
2009: Marcus Berg (Sweden)
2007: Rosyton Drenthe (Netherlands)
2006: Klaas Jan Huntelaar (Netherlands)
2004: Alberto Gilardino (Italy)
2002: Petr Cech (Czech Rep)
2000: Andrea Pirlo (Italy)
1998: Francesc Arnau (Spain)
1996: Fabio Cannavaro (Italy)
1994: Luis Figo (Portugal)
1992: Renato Buso (Italy)
1990: Davor Suker (Croatia)
1988: Laurent Blanc (France)
1986: Manuel Sanchis (Spain)
1984: Mark Hateley (England)
1982: Rudi Voeller (Germany)
1980: Anatoli Demianenko (USSR)
1978: Vahid Halilhodzic (Yugoslavia)
0 comments:
Post a Comment