Saturday, June 8, 2013

Benki ya Exim yatunukiwa tuzo ya utunzaji bora mazingira


793ea701476d5db2a4fd8cf1e0bf5880_XL
Benki ya Exim imeibuka mshindi wa jumla kwa taasisi za fedha kwenye Tuzo za Mazingira zilizoandaliwa na Manispaa ya Ilala kwa mwaka 2013.

Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango ya taasisi mbali mbali nchini katika utunzaji wa mazingira.
Sherehe za utoaji wa tuzo hizo ilifanyika jana katika viwanja wa Zakhem,
Mbagala, jijini Dar es Salaam zikiwa zimeandaliwa na wilaya ya Temeke ikiwa ni sehemu ya kuhadhimisha Siku ya Mazingira Duniani yenye kauli mbinu ya ‘Fikiri, Kula, Tunza’.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliihimiza jamii umuhimu wa kutunza mazingira wanayoishi ili kuwa endelevu.
“Mahali popote ambapo mazingira yameharibiwa hata uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara utapungua siku hadi siku,” alisema.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam una changamoto mbalimbali katika masuala ya utunzaji mazingira ikiwemo usimamizi hafifu wa  sheria ndogo ndogo za hifadhi ya mazingira.
“Kuna watu wanakiuka na wengine wanagomea lakini mkumbuke mnavyofanya hivyo mnajijengea maisha duni. Sheria hizi zinazowekwa naomba sana mzisimamie kwa manufaa ya taifa letu, hatuna budi kutii sheria hizi bila shuruti na tukifanya hivyo Dar es
Salaam yetu itakuwa sehemu nzuri sana ya kuishi,” aliongeza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Anthony Grant, mara baada ya kupokea tuzo hiyo alisema mikakati na jitihada za benki yake ni kuendelea kuunga mkono kampeni mbali mbali za utunzaji mazingira nchi nzima.
Alisema kuna umuhimu kwa wadau wote kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza nguvu katika utunzaji wa mazingira hali ambayo itasaidia kuongeza mapinduzi ya uchumi wa kijani na kuboresha maisha ya jamii na kupunguza mazingira hatarishi kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment