Sunday, June 9, 2013

AFRIKA NA KOMBE LA DUNIA: EGYPT PEKEE USHINDI ASILIMIA MIA MOJA

BRAZIL_2014_BESTLEO YAITWANGA ZIMBABWE 4-2 HUKO HARARE!
MKONGWE Mohammed AbouTrika alifunga Bao moja na Chikupizi wa FC Basel, Mohamed Salah, alipiga Hetitriki wakati Egypt ilipoiteketeza Zimbabwe huko Harare katika Mechi ya KUNDI G la Mchujo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014 na kujikita kileleni wakiwa Timu pekee Afrika ambayo imeshinda Mechi zake zote.
Egypt wanaweza kuwa Timu ya kwanza kufuzu kuingia Raundi ya Mwisho ya Mtoano ikiwa baadae leo Guinea, ambao wako Nyumbani, watashindwa kuifunga Mozambique.

MAGOLI:
Zimbabwe 2
-21 Musona
-81 Billiat
Egypt 4
-5 Mohammed AbouTrika
-41, 76 & 83 Mohamed Salah
Nchi nyingine ambazo hadi Jana zilikuwa zimeshinda Mechi zao zote ni Congo na Tunisia lakini hiyo Jana zilitibuliwa kwa kutoka Sare Congo kutoka suluhu na Gabon na Tunisia kubanwa na Sierra Leone respectively.
KUNDI G
Egypt Mechi 4 Pointi 12
Guinea Mechi 3 Pointi 4
Mozambique  Mechi 3 Pointi 2
Zimbabwe Mechi 4 Pointi 1
Kipigo hiki kimeifanya Zimbabwe iage rasmi safari ya Brazil.
RATIBA/MATOKEO:
Jumatano Juni 5
Kenya 0-1 Nigeria
Malawi 0-0 Namibia
Ijumaa Juni 7
Libya 0 Congo, DR 0
Sudan 1 Ghana 3
Jumamosi Juni 8
Uganda 1 Liberia 0
Zambia 4 Lesotho 0
Botswana 1 Ethiopia 2
Central African Republic 0 South Africa 3
Gabon 0 Congo 0
Angola 1 Senegal 1
Gambia 0 Ivory Coast 3
Sierra Leone 2 Tunisia 2
Cape Verde 2 Equatorial Guinea 1
Morocco 2 Tanzania 1
Jumapili Juni 9
Zimbabwe 2 Egypt 4
Niger v Burkina Faso
Guinea v Mozambique
Benin v Algeria
Mali v Rwanda
Togo v Cameroon

0 comments:

Post a Comment